Tausi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Tausi ni ndege wakubwa wa jenasi Pavo na Afropavo katika familia ya Phasianidae.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi ...
Tausi | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Tausi wa Kongo | ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Funga
Dume ana rangi ing’aayo ya majani au buluu na mkia wake ni mrefu mwenye rangi nyingi. Jike ana rangi inayofifia pengine kahawia tu. Jinsia zote zina ushungi. Dume hukoga mkia kwa ubembelezi.
Hula matunda, maua, wadudu na watambazi. Hutaga mayai matatu hadi manane ardhini.
Tausi wa Kongo anatokea Kongo ya Kidemokrasia. Spishi mbili nyingine zinatokea misitu ya Asia, lakini zimewasilishwa katika sehemu nyingine za dunia, hususa tausi mhindi.