Alkibiades
From Wikipedia, the free encyclopedia
Alkibiades, mwana wa Kleinias (Ἀλκιβιάδης, mnamo 450 KK - 404 KK) alikuwa mwanasiasa, mhutubu na mwanajeshi mashuhuri kutoka mjini Athini katika Ugiriki ya Kale. Alikuwa na majukumu muhimu wakati wa Vita ya Peloponesi kati ya Sparta na Athini.