Darfur Kaskazini
From Wikipedia, the free encyclopedia
Darfur Kaskazini (kwa Kiarabu: شمال دارفور, Shamal Darfor) ni mojawapo ya wilayat au majimbo 18 ya Sudan. Ni mojawapo ya majimbo yanayojumuisha kanda ya Darfur.
Lina ukubwa wa eneo wa km² 296,420 na idadi ya wakazi wake inakadiriwa kuwa 1,583,000 (2006). Al-Fashir ndio mji mkuu wake. Miji mingine muhimu ni pamoja na miji ya Kutum na Tawila.