Hifadhi ya kisiwa cha Rubondo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Hifadhi ya Rubondo inapatikana katika kisiwa kilichopo pembezoni mwa Ziwa Victoria, ambalo ni ziwa la pili kwa ukubwa duniani, likiwa linazungukwa na nchi tatu, Tanzania, Kenya na Uganda. Imeundwa na mkusanyiko wa visiwa tisa vidogovidogo.
Kisiwa cha Rubondo ni makazi na mazingira muafaka ya kuzaliana samaki wakiwemo sato na sangara. Sangara huweza kuwa na ukubwa wa hadi kilo 100.
Fukwe za kisiwa hiki ni miongoni mwa makazi ya pongo na nzohe. Aidha hifadhi hii ni maskani makuu ya ndege na samaki kama zumbuli, chechele na taisamaki.
Mbali na ndege hao kisiwa hiki ni makazi ya aina nyingine nyingi za ndege wa majini na mimea kadhaa ambayo hutoa harufu nzuri ya kuvutia.
Wanyama wakazi wa hifadhi hii ni kama viboko, pongo, nzohe, fisi maji, mamba na pimbi ambao wanashirikiana makazi na wanyama waliohamishiwa katika hifadhi hii kama sokwe, tembo, mbega weusi na weupe na twiga.