Jamestown (St. Helena)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Jamestown ni bandari na mji mkuu wa eneo la ng'ambo la Uingereza linaloundwa na visiwa vidogo vya Saint Helena, Ascension na funguvisiwa la Tristan da Cunha. Mji uko kisiwani St. Helena katika bahari ya Atlantiki takriban km 1.868 kutoka pwani ya Angola. Idadi ya wakazi inakaribia 1,000.
Mji wenyewe ni hasa barabara moja yenye nyumba za aina ya ujenzi wa kikoloni cha Kiingereza.