Lugha za Kibalti-Kislavoni
From Wikipedia, the free encyclopedia
Lugha za Kibayi-Kislavoni ni jina la kundi la lugha zinazotumika hasa katika Ulaya Mashariki na Ulaya Kusini Mashariki, lakini pia Asia Kaskazini. Kundi hilo linaainishwa kama mojawapo kati ya yale ya lugha za Kihindi-Kiulaya.
Zinagawanyika kati ya lugha za Kibalti, lugha za Kislavoni za Mashariki, lugha za Kislavoni za Magharibi na lugha za Kislavoni za Kusini.
Lugha hizo zilienea hasa katika karne ya 6 na karne ya 7 BK. Kwa sasa wasemaji wake ni kama milioni 320.