Otto von Bismarck
From Wikipedia, the free encyclopedia
Otto von Bismarck (1 Aprili 1815 – 30 Julai 1898) alikuwa mwanasiasa mashuhuri wa Ujerumani katika karne ya 19.
Akiwa waziri mkuu wa Prussia alijenga umoja wa Ujerumani katika vita tatu dhidi ya Denmark (1864), Austria (1866) na Ufaransa (1870/71).
Kama Chansella wa Dola la Ujerumani aliongoza siasa ya nchi hadi 1890 alipoachishwa na Kaisari kijana Wilhelm II.