Saint Thomas (Visiwa vya Virgin vya Marekani)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Saint Thomas ni kisiwa kikubwa cha Visiwa vya Virgin vya Marekani katika bahari ya Karibi. Kuna wakazi 51,181 na eneo la kisiwa ni 80.9 km². Mji mkuu pia makao makuu ya utawala wa Kimarekani wa eneo hili ni mji wa Charlotte Amalie.
St. Thomas ilikuwa kisiwa kikuu cha India ya Magharibi ya Kidenmark kati ya 1672 - 1917. Tangu 1917 visiwa vimeuzwa kwa Marekani. Siku hizi ni eneo la Marekani, wakazi ni raia wa Marekani lakini hawashiriki katika uchaguzi wa rais au bunge la Washington.