Tambarare ya Siberia Magharibi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Tambarare ya Siberia Magharibi (kwa Kiingereza: West Siberian Plain) ni tambarare kubwa ambayo inachukua sehemu ya magharibi ya Siberia, kati ya Milima ya Ural upande wa magharibi na Mto Yenisei upande wa mashariki, tena Milima ya Altay upande wa kusini mashariki. Eneo lote ni takriban km² 2,500,000.
Miji muhimu ni pamoja na Omsk, Novosibirsk, Tomsk na Chelyabinsk.