Uruguay
nchi katika Amerika Kusini / From Wikipedia, the free encyclopedia
Uruguay ni nchi ya Amerika Kusini upande wa mashariki ya bara kando ya Atlantiki.
Ukweli wa haraka
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Libertad o Muerte (Uhuru au Mauti) | |||||
Wimbo wa taifa: Orientales la Patria o la Tumba! | |||||
Mji mkuu | Montevideo 34°53′ S 56°10′ W | ||||
Mji mkubwa nchini | Montevideo | ||||
Lugha rasmi | Kihispania | ||||
Serikali Rais |
Jamhuri Luis Lacalle Pou | ||||
Uhuru Ilitangazwa Ilitambuliwa |
25 Agosti 1825 28 Agosti 1828 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
176,215 km² (ya 91) 1.5 | ||||
Idadi ya watu - Julai 2022 kadirio - 2011 sensa - Msongamano wa watu |
3,407,213 (ya 132) 3,286,314 19.8/km² (ya 206 1) | ||||
Fedha | Peso ya Uruguay (UYU ) | ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC-3) (UTC-2) | ||||
Intaneti TLD | .uy | ||||
Kodi ya simu | +598
- |
Funga
Uruguay ni kati ya nchi ndogo kabisa za Amerika Kusini pamoja na Surinam.
Imepakana na Brazil na Argentina. Sehemu kubwa ya mipaka ya nje ni maji: mdomo mpana wa mto Rio de la Plata uko upande wa kusini-magharibi na Atlantiki upande wa kusini-mashariki.
Mji mkuu ni Montevideo wanapoishi zaidi ya nusu ya wakazi wote wa nchi (1,900,000 kati ya 3,407,000 hivi).