Watrinitari
From Wikipedia, the free encyclopedia
Shirika la Utatu Mtakatifu (kifupi Watrinitari, kutokana na neno la Kilatini Trinitas, maana yake Utatu) ni utawa wa Kanisa Katoliki ambao ulianzishwa kwenye eneo la Cerfroid, kilometa 80 hivi kaskazini mashariki kwa Paris (Ufaransa), mwishoni mwa karne ya 12.
Mwanzilishi wake alikuwa Yohane wa Matha, ambaye alikubaliwa na Papa Innocent III kwa waraka Operante divine dispositionis clementia, uliotolewa tarehe 17 Desemba 1198.
Lengo lilikuwa kuheshimu fumbo la Utatu mtakatifu pamoja na kukomboa Wakristo waliotekwa utumwani katika vita vya msalaba.
Leo shirika lina nyumba katika nchi mbalimbali za Ulaya na Amerika, halafu Madagascar, Misri, India, Korea na Philippines.