Satiro wa Milano
From Wikipedia, the free encyclopedia
Satiro wa Milano (Trier, leo nchini Ujerumani, au Roma, Italia, 330 hivi - Milano, Italia, 378), alikuwa kaka wa Ambrosi.
Mdogo wake alipochaguliwa kuwa askofu wa Milano, Satiro aliacha cheo chake cha gavana akamsaidie yeye na dada yao Marselina aliyeamua kushika ubikira wake kwa ajili ya Mungu.
Kidogo kabla ya kufariki dunia alipata ubatizo na baada ya kufa mdogo wake alitangaza sifa zake[1].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 17 Septemba[2].