Sigimundi Felinski
From Wikipedia, the free encyclopedia
Sigimundi Szczesny Felinski (Voiutyn, leo nchini Ukraina, 1 Novemba 1822 – Krakow, Polandi, 17 Septemba 1895) alikuwa askofu mkuu wa Warsaw, mji mkuu wa Polandi, ambaye kati ya matatizo makubwa alijitahidi kupigania uhuru na upyaisho wa Kanisa, ingawa alipaswa kukaa karibu miaka yote uhamishoni.
Pia alianzisha shirika la kitawa la Masista Wafransisko wa Familia ya Maria ili kusaidia umati katika shida zao mbalimbali [1].
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 18 Agosti 2002 halafu Papa Benedikto XVI alimtangaza mtakatifu tarehe 11 Oktoba 2009.[2][3]