Stanislaus Papczynski
From Wikipedia, the free encyclopedia
Stanislaus Papczynski (18 Mei 1631 – 17 Septemba 1701) alikuwa mtawa padri wa Polandi.
Baada ya kuishi katika shirika la Waskolopi, alianzisha la kwake, Wanamaria wa Kukingiwa Dhambi Asili, ambalo lilikuwa la kwanza kuanzishwa kwa wanaume nchini Polandi[1].
Papa Benedikto XVI alimtangaza mwenye heri tarehe 16 Septemba 2007 halafu Papa Fransisko alimtangaza mtakatifu tarehe 5 Juni 2016.