Al-Masudi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Al-Masudi (kwa Kiarabu المسعودي, jina kamili أبو الحسن علي بن الحسين بن علي المسعودى , Abu Hassan'Alī ibn al-Husayn bin al-al-Mas'ūdī; 896 hivi - 956) alikuwa mwanahistoria, mwanajiografia na mpelelezi Mwarabu. Wakati mwingine huitwa "Herodoti wa Waarabu". [1] [2]
Al-Masudi alikuwa mwandishi mashuhuri kwa kuunganisha historia na jiografia ya kitaalamu katika kitabu chake kikubwa "Malisho ya Dhahabu na Migodi ya Almasi" (kwa Kiarabu مروج الذهب و معادن الجوهر, muruj adh-dhahab wa ma'adin al-jawhar) alimolenga kutoa taarifa ya historia ya dunia. Alitunga kwa jumla zaidi ya vitabu 20 kuhusu mada za kidini na utaalamu wa jumla pamoja na historia, jiografia, sayansi, falsafa na dini.[3]