Bikira Maria wa Rozari
From Wikipedia, the free encyclopedia
Bikira Maria wa Rozari ni jina mojawapo linalotumika kwa Bikira Maria kuhusiana na rozari yake.
Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 7 Oktoba[1], siku ambayo mwaka 1571 jeshi la majini la Wakristo lilifaulu kushinda lile la Waturuki Waislamu katika mapigano ya Lepanto, karibu na Ugiriki.
Ushindi huo haukutegemewa, ila uliombwa na Wakatoliki wa Ulaya nzima kwa Rozari, kama alivyoagiza Papa Pius V[2][3]. Mjini Roma mwenyewe aliongoza maandamano ya ibada kwa ajili hiyo.
Matokeo yake yakawa ya kudumu: Waturuki hawakuweza kuteka Ulaya magharibi[4] wala kwenda Amerika kupitia bahari ya Atlantiki.
Basi, Papa alianzisha sikukuu ya kila mwaka kusherehekea ushindi huo.