Denis wa Paris
From Wikipedia, the free encyclopedia
Denis wa Paris alikuwa Mkristo wa karne ya 3 kutoka Roma (Italia).
Kadiri ya wanahistoria Wakristo[1]. chini ya kaisari Decius (250 BK), Papa Fabian alituma maaskofu 7 kutoka Roma kwenda Gallia (Ufaransa wa leo) wakahubiri Injili: Grasyano huko Tours, Trofimo huko Arles, Paulo huko Narbonne, Saturnini huko Toulouse, Denis huko Paris, Austremoni huko Clermont na Martial huko Limoges.
Akiwa askofu wa Paris (Ufaransa) aliuawa pamoja na padri Eleuteri na shemasi Rustiko kwa kukatwa kichwa kwa sababu ya imani yake.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.