Fuko-dhahabu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Fuko-dhahabu | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Fuko-dhahabu mkubwa (Chrysospalax trevelyani) | ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Nusufamilia 2, jenasi 9:
| ||||||||||||||||
Mafuko-dhahabu au mafuko butu ni wanyama wa familia Chrysochloridae ambao wanachimba katika ardhi na kushinda takriban maisha yao yote chini ya uso wake. Wanyama wengine waitwao fuko ni wanafamilia wa Bathyergidae na Spalacidae (oda Rodentia), Talpidae (Soricomorpha) na Notoryctidae (Notoryctemorphia). Spishi zote za fuko-dhahabu zinatokea Afrika kusini kwa Sahara. Hula wadudu. Mafuko hawa huchimba mahandaki yao na miguu ya mbele iliyo na ukucha wa tatu ambao umevuvumulika. Vidole vya kwanza na vya nne vimebaki kama masalio na kile cha tano kimepotea. Miguu ya nyuma ina vidole vitano vyenye ngozi katikati. Macho yao hayafanyi kazi na yamefunika kwa ngozi. Masikio ni vipenyo vidogo tu.