Kiuadudu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiuadudu (pia kiuawadudu, kiuatilifu au dawa ya wadudu, kwa Kiingereza: insecticide')' ni sumu au patojeni zilizoandaliwa kuua wadudu, kuwafukuza au kuchelewesha ukuaji wao.[1] Kinaweza kulenga wadudu wenyewe, mayai au lava.
Viuadudu hutumiwa katika kilimo, tiba, tasnia na kwenye nyumba za watu. Watu hulenga kuua wadudu kwa sababu wanaweza kuharibu mali, kusababisha hatari kwa afya au kuwa na usumbufu tu. Viuadudu vinatajwa kuwa sababu muhimu ya kuongezeka kwa tija ya kilimo ya karne ya 20. [2]
Lakini matumizi ya viuadudu huwa na hatari ya kuvuruga ekolojia na hivyo kuathiri mazingira ya wanyama na mimea. Viuadudu vingi ni sumu pia kwa wanyama wasio wadudu na pia kwa binadamu. Kuna viuadudu vinavyokolea katika mfuatano wa ulishano (food chain).