Lauryn Hill
From Wikipedia, the free encyclopedia
Lauryn Noel Hill (amezaliwa tar. 26 Mei 1975) ni mshindi mara nane wa Tuzo za Grammy akiwa kama mwimbaji, rapa, mwanamuziki, mtunzi wa nyimbo, mtayarishaji wa rekodi za muziki, na mwigizaji bora wa filamu kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Lauryn Hill. Katika shughuli zake za awali, alianza kujibebea sifa kubwa katika ulimwengu wa muziki wa hip hop akiwa kama mwanamke pekee wa kundi la muziki huo la The Fugees.
Lauryn Hill | |
---|---|
Lauryn Hill akiimba mjini Ottawa mnamo 2012 | |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Lauryn Noel Hill |
Amezaliwa | 26 Mei 1975 (1975-05-26) (umri 48) |
Asili yake | East Orange, New Jersey, Marekani |
Aina ya muziki | hip hop, underground hip hop, alternative hip hop, soul, neo-soul, R&B, reggae, muziki wa asili, acoustic |
Kazi yake | Mwimbaji, rapa, mtunzi wa nyimbo, mtayarishaji wa rekodi, mwigizaji |
Ala | Sauti, gitaa, piano |
Miaka ya kazi | 1993-hadi leo |
Studio | Columbia, Ruffhouse |
Ame/Wameshirikiana na | The Fugees, Mary J Blige, Talib Kweli,Aretha Franklin |
Tovuti | Lauryn-Hill |
Mnamo 25 Agosti katika mwaka wa 1998, akaanza kufanya kazi kama msanii wa kujitegemea na kuweza kutoa albamu moja iliyompatia mafanikio makuwa kabisa. Albamu ilikwenda kwa jina la The Miseducation of Lauryn Hill, albamu iliyosaidia kuinua muziki wa neo-soul katika ngazi za kibiashara.
Baada ya miaka minne ya mapumziko, akatoa albamu ya MTV Unplugged No. 2.0 iliyorekodiwa mnamo 21 Julai 2001 katika studio za MTV. Hill ameshinda tuzo nane za Grammy na pia ni mama wa watoto watano aliozaa na Rohan Marley, mtoto wa nne wa mwanamuziki wa raggae wa zamani - Bob Marley.