Maria wa Msalaba MacKillop
From Wikipedia, the free encyclopedia
Maria wa Msalaba MacKillop (Melbourne, Australia, 15 Januari 1842 - Sydney, Australia, 8 Agosti 1909) alikuwa sista mwanzilishi mwenza wa shirika la kitawa la Masista wa Mt. Yosefu wa Moyo Mtakatifu ambalo ndani ya Kanisa Katoliki linahudumia hasa wasichana fukara wasio na elimu.
Aliongoza shirika hilo hadi kifo chake kati ya wingi wa matatizo, masingizio na dharau [1].
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 19 Januari 1995, halafu Papa Benedikto XVI akatangaza mtakatifu tarehe 17 Oktoba 2010[2], wa kwanza mzaliwa wa Australia[3][4].